Tagged Under:
JESUS WA MAN CITY RUKSA KUCHEZA DHIDI YA SPURS KESHO JUMAMOSI
By:
Unknown
On: Jumamosi, Januari 21, 2017
MANCHESTER
City sasa wameruhusiwa kumtumia Staa Mbrazil wa Miaka 19 Gabriel Jesus
kwenye Mechi yao ya EPL, Ligi Kuu England, ya kesho Jumamosi dhidi ya
Tottenham Hotspur.
City walishafikia makubaliano na Klabu
ya Brazil Palmeiras tangu Mwezi Julai Mwaka Jana kumnunua Kinda huyo wa
Brazil mwenye Miaka 19 kwa Dau la Pauni Milioni 27 na pia kukubali
Mchezaji huyo abakie Palmeiras hadi Msimu wa Brazil utakapoisha Mwezi
Desemba.
Jesus amekuwa Kambini na City kwa Wiki 3 sasa lakini
ukiritimba umekwamisha Uhamisho wake kukamilika rasmi na hivyo kusitisha
kuichezea rasmi City.
Kinda
huyo ndio kwanza amechomoza kwenye Soka la Dunia akiwa na Msimu wa Pili
tu na Palmeiras lakini akaiongoza Klabu hiyo kutwaa Ubingwa wa Taifa
Mwezi Novemba baada ya kutwaa Medali ya Dhahabu akiichezea Brazil kwenye
Michezo ya Olimpiki, RIO 2016, Mwezi Julai.
Jesus alianza kukichezea
Kikosi cha Kwanza cha Timu ya Taifa ya Brazil Mwezi Septemba Mwaka Jana
na kufunga Bao 4 katika Mechi zake 6.
Hivi sasa Man City wapo
Nafasi ya 5 kwenye EPL, wakiwa Pointi 10, nyuma ya Vinara Chelsea baada
ya kufungwa Mechi 2 kati ya 3 walizocheza mwisho.
JE WAJUA?
-Jesus alijilukana kama Gabriel Fernando alipoanza kuichezea Palmeiras akiwa na Miaka 17.
-Akiwa
huko alipewa Jezi Namba 33 [Umri wa Yesu Kristu] na mmoja wa Maafisa
Habari wa Klabu hiyo akammwambia atumie Jina la Gabriel Jesus.
-Akiwa na Man City, Jesus pia atavaa Jezi Namba 33 ambayo awali ilivaliwa na Nahodha wa City Vincent Kompany.
0 maoni:
Chapisha Maoni