



Mapema Leo Kiungo wa Chelsea Cesc Fabregas aliibuka na kukana ripoti kuwa yeye ndio ameandaa maasi kwenye Timu.
Chelsea, ambao ni Mabingwa Watetezi wa Ligi Kuu England, hivi sasa wamekumbwa na matokeo mabovu baada ya kufungwa Mechi 6 kati ya 11 za Ligi Msimu huu.

Nae Nahodha wa Chelsea, John Terry, akihojiwa na kuulizwa ikiwa ni kweli yupo Mchezaji wa Chelsea alietamka kwamba ‘wapo tayari kufungwa kuliko kushinda chini ya Mourinho’, alijibu: “Katika maisha yangu yote ya Soka sijasikia Mchezaji atoke na kusema hivyo. Nakuhakikishia sisi tupo Asilimia 100 nyuma ya Meneja.”
Terry aliongeza: “Tuko pamoja, yeyote alieona Gemu zetu 4 au 5 zilizopita aliona tulikosa sana bahati. Tutageuza mambo. Tutabaki pamoja.”


0 maoni:
Chapisha Maoni