LIGI
KUU VODACOM, VPL [Vodacom Premier League], inaanza Jumamosi kwa Mechi 7
na Jumapili Mabingwa Yanga kushuka Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam
kucheza na Coastal Union. Hiyo Jumamosi, Washindi wa Pili wa VPL, Azam FC, wako kwao Azam Complex, huko Chamazi kwenye Viunga vya Jiji la Dar es Saalam kucheza na Prisons wakati Vigogo Simba kusafiri kwenda Mkwakwani, Tanga kuivaa African Sports iliyopanda Daraja Msimu huu.
Mechi nyingine ni Ndanda FC ya Mtwara kuwa wenyeji wa Mgambo Shooting Uwanjani Nagwanda Sijaona mjini Mtwara, Wana Lizombe Majimaji wakiwa wenyeji wa Maafande wa JKT Ruvu katika Uwanja wa Majimaji mjini Songea.
Stand
United FC watawakaribisha Mtibwa Sugar katika Uwanja wa Kambarage mjini
Shinyanga, Toto Africans watawakaribisha Mwadui FC Uwanja wa CCM
Kirumba na Mbeya City watacheza na Kagera Sugar katika Uwanja wa Sokoine
jijini Mbeya. Jumapili VPL itaendelea kwa mchezo mmoja tu utakaochezwa katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es salaam ambapo Mabingwa Watetezi Yanga watawakribisha Wagosi wa Kaya Coastal Union.
0 maoni:
Chapisha Maoni