.

.

.

.

.

.

.

,

,

.

.

Jumamosi, 12 Septemba 2015

Tagged Under:

Serena Williams apoteza ushindi kwenye mechi ya U.S Open, Drake alaumiwa…!!

By: Unknown On: Jumamosi, Septemba 12, 2015
  • Share The Gag


  • Staa wa mchezo wa Tennis, Serena Williams na superstaa wa muziki wa Hip hop Drake wamekuwa topic kwenye mitandao mingi baada ya tetesi nyingi kusambaa kuwa wawili hao wapo kwenye mahusiano ya kimapenzi.
    drake
    Yote yalianza siku ambayo mapaparazzi walimnasa Drake kwenye picha akiwa kwenye mashindano ya Serena Williams huko Australia… haikuishia hapo, baada ya Serena kushinda Australia Open Championships, Drake alionekana tena kwenye mashindano yake ya French Open (Roland Garros), Wimbledon na haya ya jana U.S Open Championships.
    drake2
    Sasa jana staa huyo wa tennis aliweka headlines tofauti baada ya kukosa ushindi kwenye U.S Open dhidi ya Roberta Vinci wa Italy… Cha kushangaza zaidi mashabiki wamemshambulia Drake na kumlaumu sana kwa kitendo cha Serena Williams kukosa ushindi huo!
    drake5
    Mashabiki wanadai kuwa Drake amekuwa kikwazo kwenye mashindano haya na amemchanganya sana Serena kiasi cha kumfanya ashindwe kuweka akili yake yote kwenye mashindano hayo, mashindano ambayo kama Serena Williams angeshinda basi angeweka historia ya kuwa mwanamke mweusi kushinda mashinano yote hayo kwa mfululizo!
    drake4
    Nimefanikiwa kuzinasa baadhi ya tweets za mashabiki kwenye Twitter wengi wanatumia hashtag ya #BlameDrake kuelezea hisia zao..

    0 maoni:

    Chapisha Maoni