
Vicente Del Bosque anaamini David de Gea anapaswa kufurahia mvutano huo kati ya Klabu kubwa kabisa Barani Ulaya.
De Gea alikuwa kwenye sakata la kuhamia Real Madrid lakini Uhamisho huo ulikwama Sekunde za mwisho hapo Agosti 31 baada ya Real Madrid kuchelewa kumsajili kwa wakati kwenye Mtandao wa FIFA wa Uhamisho wa Kimataifa, TMS [Transfer Matching System] na pia LFP, La Liga na kuziacha Klabu hizo mbili zikilaumiana.
Del Bosque amesema: “Lazima afurahie kwani Klabu kubwa zilikuwa zikimgombea. Sijaongea nae peke yake. Lakini anapaswa kufanya mazoezi. Yupo sehemu salama.”

Hivi sasa De Gea yuko kwenye Timu ya Taifa ya Spain ikijitayarisha kucheza Mechi za Kundi lao la EURO 2016 Wikiendi hii dhidi ya Macedonia na Slovakia.

0 maoni:
Chapisha Maoni