
Full time, Arsenal 0 vs 2 West Ham United
Meneja mpya Slaven Bilic ameanza Ligi Kuu England kwa kuiongoza Timu yake West Ham kuitandika Arsenal 2-0 kwenye Dabi ya Jiji la London huko Emirates na kumfanya Meneja wa Arsenal Arsene Wenger kutoamini kilichomkuta na kubaki kushika kichwa, West Ham, ambao walimchezesha Kijana wa Miaka 16 Reece Oxford, walifunga Bao lao la kwanza baada ya Kipa wa Arsenal Petr Cech kuitokea Frikiki na kuikosa na kumruhusu Cheikhou Kouyate kufunga kwa kichwa katika Dakika ya 43.
Nafasi pekee waliyokaribia Arsenal kufunga katika Kipindi cha Kwanza ni pale Aaron Ramsey alipopiga Posti.



0 maoni:
Chapisha Maoni