.

.

.

.

.

.

.

,

,

.

.

Jumatatu, 10 Agosti 2015

Tagged Under:

MIKE DEAN NDIE REFA WA MTANANGE WA LEO KATI YA WEST BROM vs MANCHESTER CITY HUKO HAWTHORNS USIKU.

By: Unknown On: Jumatatu, Agosti 10, 2015
  • Share The Gag

  • Leo Usiku Mabingwa wa zamani wa England Manchester City wanaingia Ugenini The Hawthorns kucheza na West Bromwich Albion katika Mechi yao ya kwanza kabisa ya Msimu mpya wa Ligi Kuu England.
    Hii ni Mechi ya mwisho ya Raundi ya kwanza kwa Timu 20 za Ligi Kuu England ambazo zilianza mbio zao za Msimu mpya hapo Jumamosi na Jana Jumapili huku ikishuhudiwa Mabingwa Chelsea kutoka Sare 2 kwa 2 na Swansea City, Man United kuifunga Spurs 1-0 na Arsenal wakitandikwa kwao Emirates 2-0 na West Ham.Hali za Wachezaji
    West Brom, chini ya Meneja Tony Pulis, huenda wakamkosa Beki wao ambae ni Mchezaji wa zamani wa Man City, Joleon Lescott, ambae ana maumivu lakini Wachezaji wao wapya, Rickie Lambert, James McClean na James Chester wapo tayari kucheza isipokuwa Serge Gnabry kutoka Arsenal ambae Uhamisho wake haukukamilika kwa wakati.
    Manchester City, chini ya Meneja Manuel Pellegrini, itawakosa Gael Clichy na Fabian Delph wote wakiwa na maumivu lakini David Silva, Samir Nasri na Sergio Aguero, ambao walikuwa wagonjwa, wako fiti kuanza Mechi hii.

    Uso kwa Uso
    -Manchester City hawajafungwa na WBA katika Mechi zao 5 zilizopita Uwanjani The Hawthorns, wakishinda 4 kati ya hizo.
    -City, wakicheza kwao Etihad na hapo The Hawthorns, wameifunga WBA mara 7 mfululizo.

    Mike Dean refa atakayechezesha mpambano huo utakaopigwa usiku huu saa nne kamili kwa saa za hapa Tz.
    Referee: Mike Dean Assistants: S Long, M Perry Fourth Official: M Clattenburg 
    LIGI KUU ENGLAND
    Jumatatu Agosti 10

    22:00 West Brom v Man City
    Ijumaa Agosti 14
    22:45 Aston Villa v Man United
    Jumamosi Agosti 15
    14:45 Southampton v Everton
    17:00 Sunderland v Norwich
    17:00 Swansea v Newcastle
    17:00 Tottenham v Stoke
    17:00 Watford v West Brom
    17:00 West Ham v Leicester

    0 maoni:

    Chapisha Maoni