Tagged Under:
KIINGILIO CHA MTANANGE WA YANGA NA PLATINUM FC CHA CHINI NI 5,000/ MPAKA 30,000.
By:
Unknown
On: Ijumaa, Machi 13, 2015
KIINGILIO cha chini katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika baina ya Yanga SC na Platinum FC ya Zimbabwe kitakuwa na Sh. 5,000 kwa jukwaa la viti vya rangi bluu na kijani
Yanga
wataikaribisha Platinum FC ya Zimbabwe katika mchezo wa kwanza wa
raundi ya kwanza ya Kombe la Shirikisho Afrika utakaochezwa Uwanja wa
Taifa, Dar es Salaam, jumapili.
Mkuu wa Idara ya Habari na
Mawasiliano ya Yanga SC, Jerry Muro alisema kwamba, katika jukwaa la
viti vya Rangi Chungwa itakuwa Sh, 7000, VIP C Sh. 15,000, VIP B Sh.
20,000, na VIP A Sh 30,000.
Muro
amesema tiketi zitaanza kuuzwa Jumamosi Saa 2:00 asubuhi katika vituo
vya Karume (Ofisi za TFF), Mgahawa wa Steers (Posta Mpya), Oilcom
(Buguruni), BigBon (Kariakoo), Olicom (Ubungo), Dar Live (Mbagala),
Uwanja wa Uhuru, Kivukoni (Ferry) na Makumbusho (kituo cha mabasi).

Aidha, amesema magari yenye vibali maalum ndiyo yatakayoruhusiwa kuingia ndani ya Uwanja siku hiyo.
Yanga SC imefika hatua hii baada ya kuitoa BDF XI ya Botswana, wakati Platinum iliing’oa Sofapaka ya Kenya.
Wakati
huo huo: Kikosi cha Platinum kilichotarajiwa kuwasili Saa 2:00 usiku wa
leo, hakijawasili na wenyeji wao, Yanga SC wameshangaa kwa sababu
hawana taarifa nyingine.
0 maoni:
Chapisha Maoni