
Arsenal Mabingwa 2015 FA Community Shield

Alex Oxlade akipeta baada ya kufunga bao

Chamberlain akishangilia vikali juu kwa juu

Mbele ya Mashabiki
Msimu
mpya wa Soka huko England umeanza rasmi hii Leo kwa Mechi maalum ya
kugombea Ngao ya Jamii kati ya Mabingwa wa England Chelsea na waliobeba
FA CUP Arsenal Uwanjani Wembley Jijini London na Arsenal kuibuka kidedea
kwa kuifunga Chelsea 1-0 ikiwa ni ishara maalum Msimu huu wametangaza
nia ya kutwaa Ubingwa.
Huu ni ushindi wa kwanza kwa Arsenal,
chini ya Meneja Arsene Wenger, dhidi ya ya Chelsea, chini ya Meneja Jose
Mourinho, ambao washakutana uso kwa uso mara 13 na Chelsea kushinda
mara 7 na Sare 6.
Alex Oxlade-Chamberlain alifunga Bao
pekee na la ushindi kwa Arsenal katika Dakika ya 24 alipopokea pande
zuri toka kwa Theo Walcott na hilo ni Bao la kwanza kabisa dhidi ya
Chelsea, chini ya Meneja Jose Mourinho, tangu 2007.
Alex Oxlade Chamberlain akipongezwa

Cazorla na Chamberlain

Kocha wa Timu ya Chelsea Jose Mourinho akijionea Vijana wake Wembley

Theo Walcott akigombea mpira wa Kichwa dhidi ya kipa wa Chelsea

Monreal nae kwenye patashika mpira wa kichwa

Chupuchupu langoni mwa Arsenal Petr Cech akiokoa
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni