Klabu 3 za Ligi Kuu England zitacheza huko Bara la Asia, Singapore, kugombea Kombe la Ligi Kuu Asia, 2015 Premier League Asia [Barclays Asia Trophy], pamoja na Kombaini ya Wenyeji kuanzia Jumatano hii.
Mashindano haya ya 7 yatazishirikisha Klabu za Arsenal, Everton, Stoke City na Kombaini ya Singapore.
Mechi zote zitachezwa ndani ya Singapore National Stadium, Mjini Singapore kuanzia Julai 15 hadi 18.
Katika Mechi za kwanza Everton itacheza na Stoke City na Arsenal kuivaa Kombaini ya Singapore.
Washindi wa Mechi hizo watacheza Fainali wakati Timu zilizofungwa zitacheza Mechi yao kusaka Mshindi wa Tatu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni