Ijumaa, 2 Oktoba 2015

VAN PERSIE AIONGOZA FENERBAHCE KUPATA SARE YA UGENINI EUROPA LEAGUE


Feneberhce ya Uturuki imejitutumua ikiwa ugenini Glasgow na kufanikiwa kupata sare ya mabao 2-2 katika michuano ya Kombe la Europa.

Ikiongozwa na Robin van Persie, Feneberhce ililazimika kusawazisha ikitoka chini kwa mabao 2-0 hadi kuwa 2-2.

Shuja alikuwa ni Fernandao ambaye alifunga mabao yote mawili ya kusawazisha katika dakika za 43 na 48.



Hakuna maoni:

Chapisha Maoni