.

.

.

.

.

.

.

,

,

.

.

Jumanne, 15 Septemba 2015

Tagged Under:

MTANZANIA AENDELEA KUTESA KENYA, SASA ATAKA TIMU YAKE IENDE TANO BORA

By: Unknown On: Jumanne, Septemba 15, 2015
  • Share The Gag
  • NAFTAL (KATIKATI) AKIFANYA YAKE LIGI KUU KENYA

    Beki wa zamani wa Simba, David Naftal ameendelea kung’ara katika kikosi cha Kenya Revenue Authority (KRA) na sasa amepania kuhakikisha wanamaliza Ligi Kuu Kenya wakiwa katika nafasi tano za juu.



    Kutoka Kenya, akizungumza na SALEHJEMBE, Naftal amesema amekuwa akipambana na sasa ana uhakika wa namba katika kikosi cha kwanza, lakini kwa pamoja KRA wanataka nafasi hizo tano za juu.

    “Tupo katika nafasi ya saba ya ligi. Tumebakiza mechi nne, sasa tunapambana kumaliza katika top 5.

    “Huku Kenya mkimaliza top 5, mnapata nafasi ya kucheza michuano ya Top 8 ambayo bingwa wake hucheza michuano ya Shirikisho,” alisema Naftal.

    Kwa sasa amekuwa akicheza nafasi ya kiungo mkabaji nan dye tegemeo katika kikosi hicho cha wakusanya kodi wa Kenya.

    0 maoni:

    Chapisha Maoni