JACK WILSHERE KURUDI DIMBANI BAADA WIKI 2, ROSICKY NJE MIEZI 2 NI BAADA YA KUPASULIWA MGUU!
MENEJA
wa Arsenal Arsene Wenger amesema Jack Wilshere atarejea Uwanjani baada
ya Wiki 2 baada ya kujiuguza Enka yake lakini Kiungo wao mwingine Tomas Rosicky atakuwa nje kwa Miezi Miwili baada ya kupasuliwa Goti lake.
Wilshere,
mwenye Umri wa Miaka 23, aliumia Enka ambayo ilipata ufa kwenye mfupa
wake Mazoezini hapo Agosti 1 na ilidhaniwa atakuwa nje kwa kipindi cha
hadi Miezi Miwili.
Lakini Wenger amesisitiza wao walitegemea atapona ndani ya Wiki 4 na kwa sasa mambo yako sawa.
Akiongea
na Wanahabari kabla Arsenal kucheza Ugenini na Crystal Palace hapo
Jumapili kwenye Mechi yao ya pili Ligi Kuu England baada ya kuchapwa 2-0
katika Mechi yao ya kwanza na West Ham, Wenger amesema: “Tulisema Jack
atakuwa nje kwa Wiki 4 na sasa ni Wiki ya pili.”
Lakini
habari si njema kwa Kiungo wao Rosicky mwenye Miaka 34 ambae aliumia
wakati akiichezea Nchi yake Czech Republic dhidi ya Iceland kwenye Mechi
ya Makundi ya EURO 2016 Mwezi Juni ambae sasa amefanyiwa operesheni ya
Goti na Wenger kuthibitisha atakuwa nje kwa muda mrefu unaodhaniwa kuwa
Zaidi ya Miezi Miwili.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni