
Kamati ya nidhamu ya FIFA ilifanya kikao chake nchini Canada na kufikia uamuzi huo baada ya kutizama video inayomuonesha Njoku akimpiga kumbo mchezaji wa Australia Sam Kerr katika mechi ya makundi ya kombe la dunia la wanawake .Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20 alikuwa mchezaji wa akiba na aliingia uwanjani katika dakika ya 52 ya mechi hiyo ya kombe la dunia.
Mchezaji huyo amepigwa faini ya dola elfu tatu na mia mbili $3,200.
The Super Falcons ya Nigeria iliambulia kichapo cha mabao 2-0 katika mechi hiyo.

Haijulikani kwanini hatua sawa na hiyo haikuchukuliwa dhidi ya mshambulizi wa Ufaransa Camille Abily aliyempiga kumbo mlinzi wa England Laura Bassett.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni