DKT. MAGUFULI NA MH. SULUHU WAPOKELEWA KWA SHANGWE ZANZIBAR
Wananchi na Wafuasi wa chama cha Mapinduzi CCM wakiwapokea kwa shangwe
Mgombea Urais kwa tiketi ya chama hicho Dkt John Pombe Magufuli na
Mgombea mwenza Mh.Samia Suluhu Hassan mapema asubuhi hii mara baada ya
kuwasili mjini Unguja -Zanzibar kujitambulisha kwa chama na Wananchi kwa
ujumla. Mgombea
wa Urais kwa tiketi ya CCM Dk. John Pombe Magufuli akiwa kwenye gari la
wazi pamoja na mgombea mwenza Mhe.Samia Suluhu Hassan kwenye mitaa ya
Michenzani Zanzibar. Mhe. Magufuli aliwasili Zanzibar kwa lengo la
kutambulishwa kwa wanachama wa CCM Zanzibar akiongozana na mgombea
mwenza Mhe.Samia Suluhu Hassan ambapo wote kwa pamoja walipata
kuwasalimia wananchi wa Zanzibar kwenye viwanja vya Afisi Kuu ya CCM
Zanzibar. Maelfu
ya watu wakiufuata msafara wa mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM Mhe.
John Pombe Magufuli aliyeongozana na mgombea mwenza Mhe. Samia Suluhu
Hassan. Mgombea
wa Urais kwa tiketi ya CCM Dk.John Pombe Magufuli akivishwa skafu na
chipukizi wa CCM Zanzibar mara baada ya kuwasili Afisi Kuu ya CCM
Zanzibar. Mgombea
Mwenza kwa tiketi ya CCM Mhe. Samia Suluhu Hassan akivishwa skafu na
chipukizi wa CCM nje ya jengo la Afisi Kuu ya CCM Zanzibar. Mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM Dk.John Pombe Magufuli akisalimiana na wazee maarufu wa Zanzibar Mhe.
Magufuli akiwasili kwenye kaburi la muasisi wa Mapinduzi na Rais wa
Kwanza wa Serikali Mapinduzi ya Zanzibar ,Hayati Sheikh Abeid Amani
Karume Mgombea
wa Urais kwa tiketi ya CCM Dk.John P.Magufuli pamoja na mgombea mwenza
Mhe. Samia Suluhu Hassan wakiomba dua mbele ya kaburi la Hayati Abeid
Aman Karume muasisi wa Mapinduzi ya Zanzibar. Mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM Dk. John Pombe Magufuli akisaini kitabu cha Wageni kwenye Afisi Kuu ya CCM Zanzibar. Makamu
Mwenyekiti wa CCM (Zanzibar) na Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Mgombea wa Urais kwa
tiketi ya CCM Dk. John Magufuli nje ya Afisi Kuu ya CCM Zanzibar kwenye
sherehe fupi ya kutambulishwa wagombea wa CCM kwa wanachama wa CCM. Makamu
Mwenyekiti wa CCM (Zanzibar) na Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Mgombea Mwenza Mhe. Samia
Hassan Suluhu.
Mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM Mhe. John Magufuli akiwasalimu
wananchi waliojitokeza kwenye sherehe fupi za kumtambulisha kwenye
viwanja vya Afisi Kuu CCM Zanzibar.
Kila mtu alitaka kumgusa.
Mgombea
Urais kwa tiketi ya CCM Dk.John Pombe Magufuli akiwasalimia wakazi wa
Zanzibar waliojitokeza kwa wingi kwenye viwanja vya Afisi Kuu Zanzibar
kwenye sherehe fupi ya kumtambulisha kwa wanachama pamoja na mgombea
mwenza Mhe. Samia Suluhu Hassan,kulia ni Makamu Mwenyekiti wa
CCM(Zanzibar) na Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe.Ali Mohamed
Shein. Wananchi wakishangilia. Makamu
Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
Dk.Ali Mohamed Shein akihutubia wakazi wa Zanzibar waliojitokeza kwa
wingi kushuhudia sherehe fupi za kutambulishwa kwa wagombea wa nafasi ya
Urais kwa kupitia CCM kwenye viwanja vya Afisi Kuu. Mgombea
mwenza wa nafasi ya Urais Mhe. Hassan Suluhu Hassan akizungumza kwenye
sherehe fupi za utambulisho nje ya Afisi kuu ya CCM Zanzibar. Mgombea
wa Urais kwa tiketi ya CCM Dk.John Magufuli akiwasalimu wakazi wa
Zanzibar waliojitokeza kwa wingi kwenye sherehe za kumtambulisha yeye na
mgombea mweza kwenye viwanja vya Afisi Kuu Zanzibar. Wakazi
wa Zanzibar wakimsikiliza mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM Dk. John
Magufuli kwenye viwanja vya Afisi Kuu ya CCM Zanzibar.
Makamu Mwenyekiti wa CCM (Zanzibar) Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akiagana na mgombea wa ueais kwa kupitia
CCM Dk.John Magufuli.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni