EFL CUP – NUSU FAINALI: SOUTHAMPTON 1 v 0 LIVERPOOL
Southampton
imeifunga Liverpool 1-0 huko Saint Mary hapo Jana katika Mechi yao ya
Kwanza ya Nusu Fainali ya EFL CUP, ambalo ndio Kombe la Ligi huko
England.
Juzi, kwenye Mechi nyingine ya Kwanza ya
Nusu Fainali nyingine iliyochezwa Old Trafford, Manchester United
iliichapa Hull City Bao 2-0 kwa Bao za Juan Mata na Marouane Fellaini. Bao
la ushindi la Southampton, ambao ni maarufu kama ‘Watakatifu’, hapo
Jana lilifungwa na Nathan Redmond baada kupokea Pasi ya Jay Rodriguez
katika Dakika ya 20. Southampton
wamgeweza kupata Bao nyingi kama si ushujaa wa Kipa wa Liverpool Loris
Karius alieokoa Mipira mingi na hasa mara 2 kufuta kwenye chaki ya Goli
Mipira ya Nathan Redmond. Nusu
Fainali hizi huchezwa kwa Mikondo Miwili ya Nyumbani na Ugenini na
hivyo Marudiano ya Mechi hizi yatakuwa hapo Januari 25 na 26 huko
Anfield na KCOM Stadium. EFL CUP Nusu Fainali MARUDIANO Jumatano Januari 25 23:00 Liverpool v Southampton [0-1] Alhamisi Januari 26 22:45 Hull City v Manchester United [0-2]
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni