EFL CUP
Nusu Fainali
Ratiba/Matokeo:
Jumanne Januari 10
Manchester United 2 Hull City 0
Jumatano Januari 11
22:45 Southampton V Liverpool
Manchester
United, ikiongozwa na MenejaJose Mourinho, wamepiga hatua kubwa
kuelekea kutwaa Taji kubwa la pili Msimu huu baada ya Jana huko kwao Old
Trafford kuichapa Hull City 2-0 katika Mechi ya Kwanza ya Nusu Fainali
ya EFL CUP, ambalo ndio Kombe la Ligi huko England.
Mwanzoni mwa Msimu, Man United walitwaa Ngao ya Jamii.
Bao za Man United, waliochezesha karibu Kikosi chao chote, zilifungwa na Juan Mata na Marouane Fellaini alieanzia Benchi.
Bao
la Mata lilifungwa Dakika ya 56 alipounganisha Kichwa cha Henrikh
Mkhitaryan na la pili Dakika ya 87 kupitia Fellaini alieunganisha Krosi
ya Matteo Darmian.
Hull City na Man United zitarudiana huko KCOM Stadium hapo Januari 28.
Leo Jumatano Januari 11 itachezwa Nusu Fainali ya Pili huko Saint Mary kwa Southampton kucheza na Liverpool.
Nusu Fainali hizi huchezwa kwa Mikondo Miwili ya Nyumbani na Ugenini na hivyo Marudiano ya Mechi hizi yatakuwa hapo Januari 25 na 26 huko Anfield na KCOM Stadium.
EFL CUP
Nusu Fainali
MARUDIANO
Jumatano Januari 25
23:00 Liverpool v Southampton
Alhamisi Januari 26
22:45 Hull City v Manchester United [0-2]
Nusu Fainali
Ratiba/Matokeo:
Jumanne Januari 10
Manchester United 2 Hull City 0
Jumatano Januari 11
22:45 Southampton V Liverpool

Mwanzoni mwa Msimu, Man United walitwaa Ngao ya Jamii.




Nusu Fainali hizi huchezwa kwa Mikondo Miwili ya Nyumbani na Ugenini na hivyo Marudiano ya Mechi hizi yatakuwa hapo Januari 25 na 26 huko Anfield na KCOM Stadium.
EFL CUP
Nusu Fainali
MARUDIANO
Jumatano Januari 25
23:00 Liverpool v Southampton
Alhamisi Januari 26
22:45 Hull City v Manchester United [0-2]
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni