






Bao za Man United zilifungwa na Anthony Martial Dakika ya 47 na Swansea
kurudisha Dakika ya 70 kwa Bao la Gylfi Sigurdsson lakini Wayne Rooney, akipokea pasi safi ya Martial, alifunga Bao la ushindi kwa kisigino katika Dakika ya 77.
Bao hilo limemfikisha Rooney Nafasi ya Pili katika Ufungaji Bora kwenye Ligi Kuu England, akiwa nyuma ya Alan Shearer na pia Nafasi ya Pili katika Ufungaji Bora katika Historia ya Man United akiwa na Bao 238, Bao 11 nyuma ya Mshikilia Rekodi, Sir Bobby Charlton.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni