REAL WAITISHA MKUTANO WA WANAHABARI LEO, WAMZUNGUMZIA MENEJA BENITEZ, WATAKA MABADILIKO HARAKA!!
RAIS
wa Real Madrid Florentino Perez ameitisha Mkutano na Wanahabari
utakaofanyika Leo Saa 3 na Nusu Usiku kwa Saa za Bongo na hili limekuja
mara baada ya Jumamosi kutandikwa 4-0 na Barcelona kwenye El Clasico
iliyochezwa Nyumbani kwao Santiago Bernabeu.
Wakati Real
inacharangwa na Barca Juzi Jumamosi, Mashabiki wa Real waliokuwepo
Uwanjani Bernabeu walimtaka Perez ajiuzulu lakini hili Leo halitegemewi
na hata kutimuliwa Kocha Rafa Benitez nako hakutarajiwa.
Wadau
wengi wa Real wanamlaumu Perez kwa kuingilia upangaji Timu na
kung’ang’ania kuchezeshwa Wachezaji wakubwa hata kama wamedorora na
kuachwa Wachezaji ambao wako kwenye fomu.
Mwaka 2006, Mashabiki walimgeukia na kumsakama Perez ambae ghafla alibwaga manyanga na kuachia wadhifa wake wa Urais.
Mkutano huo wa Leo na Wanahabari umekuja baada ya mapema Leo Bodi ya Real kuketi kutafakari kipigo chao kutoka kwa Barca.
Ushindi
wa Barca wa Jumamosi umewafanya wawe Pointi 6 kileleni mbele ya Real
ambapo wameporomoka hadi Nafasi ya 3 baada ya Atletico Madrid Jana
kuifunga Real Betis 1-0 na kushika Nafasi ya Pili.
Benitez,
aliewahi kuzifundisha Valencia, Liverpool, Inter Milan, Chelsea na
Napoli, ni Meneja wa 10 chini ya himaya ya Perez na alitwaa wadhifa huo
mwishoni mwa Msimu uliopita kutoka kwa Carlo Ancelotti. Ikiwa
Benitez atatimuliwa, Wadau wengi wanahisi Gwiji la France Zinedine
Zidane, ambae sasa anaifundisha Timu B ya Real, ndie atakaepewa Timu.
Mechi
inayofuata kwa Real ni hapo Jumatano Ugenini huko Ukraine wakicheza na
Shakhtar Donetsk katika Mechi ya Kundi A la UEFA CHAMPIONS LIGI ambao
wao washafuzu kuingia Raundi ya Mtoano ya Timu 16 huku wakiwa na Mechi 2
mkononi.
Ikiwa Real wataifunga Shakhtar basi watajihakikishia kufuzu toka Kundi A wakiwa ndio Vinara.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni