KLABU YA MAN UNITED NDIO KINARA KUTOA WACHEZAJI WENGI WA KIMATAIFA ULAYA!
Manchester
United ndio inaongoza kwa kutoa Wachezaji wengi wa Kimataifa kwa huko
England na pia Barani Ulaya.Msimu huu, Wachezaji wengi wameteuliwa
kuzichezea Timu zao za Taifa na Wachezaji wanaocheza Ligi Kuu England
ndio wanaongoza kwa Ulaya huku Man United wakiwa juu kwa kutoa Wachezaji
wengi zaidi.
Kwa mujibu wa Takwimu za CIES Football Observatory
Digital Atlas, Asilimia 41 ya Wachezaji waliocheza Ligi Kuu England
Msimu huu wamechezea pia Timu zao za Taifa Msimu huu huu.
Man United
wapo juu kwa kutoa Wachezaji Asilimia 72 ya wale walioteuliwa na Meneja
wao Louis van Gaal kucheza Mechi za Ligi Kuu England Msimu huu ambao
pia waliteuliwa kucheza Timu zao za Taifa.
Ijumaa
iliyopita, Wachezaji wa Man United waliovaa Jezi za Nchi zao ni Michael
Carrick, Phil Jones, Chris Smalling, Wayne Rooney na Juan Mata ambao
walicheza wakati Spain inaichapa England 2-0, wakati Anthony Martial na
Morgan Schneiderlin walikuwa kwenye France iliyoichapa Germany ambayo
ilikuwa nayo Bastian Schweinsteiger huku Daley Blind akiichezea
Netherlands na Matteo Darmian akiichezea Nchi yake Italy.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni