
Kipigo hicho kimeigandisha Villa mkiani mwa Ligi ikiwa na Pointi 4 tu kwa Mechi 11 wakati Spurs imepanda hadi Nafasi ya 5.
Spurs walikuwa mbele kwa Bao 2-0 kwa Bao za Mousa Dembele na Dele Alli hadi Mapumziko.
Kipindi cha Pili Villa walifunga Bao kupitia Kijana wa Ghana Jordan Ayew lakini katika Dakika za Majeruhi Harry Kane akafunga Bao la 3 na kuwapa Spurs ushindi wa 3-1. Mechi ya kwanza kwa Meneja mpya Remi Garde ni Jumapili Novemba 8 wakati Villa itakapokuwa Nyumbani Villa Park kuwakaribisha Vinara wa Ligi Man City.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni