WILFRED LWAKATARE WA CHADEMA AIBUKA KIDEDEA UBUNGE BUKOBA MJINI.
Hatimaye
Mkurugenzi wa ulinzi na usalama wa chama cha demokrasia na maendeleo
-Chadema Bw. Wilfred Muganyizi Lwakatare ameibuka kidedea leo hii kuwa
Mbunge wa Bukoba Mjini akiibuka kidedea dhidi ya aliyekuwa Mbunge wa
Jimbo la Bukoba Mjini kwa tiketi ya CCM, Khamis Kagasheki. Matokeo hayo
yametanga usiku huu punde na Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Bukoba mjini
Bw. Aron T. Kagurumjuli. Kura za Udiwani Chadema/ Ukawa imeshinda Kata zifuatazo: Kahororo, Kagondo, Kibeta, Kitendaguro, Nshambya, Hamugebe, Kashai, Bakoba na Bilele. CCM imepata Kata ya Rwamishenye, Buhembe, Miembeni, Nyanga na Ijunganyondo. Picha na Faustine Ruta, Bukoba
Msimamizi
wa Uchaguzi Jimbo la Bukoba mjini Bw. Aron T. Kagurumjuli akitoa
matokeo usiku huu wa saa 2:30 na kumtangaza Lwakatare kwamba ndie
mshindi na Nafasi hiyo ya Ubunge Bukoba Mjini.
Bw. Aron T. Kagurumjuli (Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Bukoba mjini) akiendelea na zoezi la kutangaza matokeo usiku huu.
Mshindi
wa nafasi ya Ubunge wa Bukoba Mjini Bw. Wilfred Muganyizi Lwakatare
kupitia Chama cha CHADEMA akifurahia baada ya kuibuka kidedea katika
kinyang'anyiro hicho baada ya kumwangusha mgembea mwenza aliyekuwa
Mbunge wa Jimbo hilo la Bukoba Mjini kwa tiketi ya CCM, Khamis Sued
Kagasheki usiku huu. Picha na Faustine Ruta, Bukoba
LICHA
ya kuonekana kana kwamba hapakuwa na dalili zozote za fujo wakati wa
zoezi la upigaji kura za Ubunge na udiwani, hali ilibadilika leo
jumatatu asubuhi baada ya wafuasi wa chama cha Chadema kutaka matokeo
mapema baada ya kupata matokeo hayo usiku wa kuamkia leo hii kuwa
Chadema imeshinda katika Kata 9 kati ya 14 wafuasi hao waliandamana
katika maeneo ya mji wa Bukoba wakitaka majibu yatolewe mapema. Kitu
ambacho hakikufanyika na Jioni hii kuleta kasheshe na ghasia. Hali hiyo
ilisababisha polisi wa kutuliza ghasia kuingilia kati na kuwatawanya
vijana hao ambao mpaka usiku huu walikuwa wamepandwa na jazba katika
eneo la ofisi za Halmashauri ya Bukoba. Vurugu zikiwemo kurushiana mawe
zilitokea. Ndipo polisi walitumia mabomu ya machozi kuwatawanya wananchi
waliokusanyika katika Ofisi za Halmashauri na kuanza kurusha mawe
wakishinikiza kutangazwa kwa matokeo ya ubunge. Hali hiyo ilitulia baada
ya Viongozi wa Chadema kuwatuliza na ndipo Matokeo yakatangazwa.
Taarifa
zinasema kuwa kulikuwa na mchuano mkali kati ya wagombea hao wawili
ambao ni Wilfred Lwakatare wa chama cha Chadema na aliyekuwa Mbunge wa
Bukoba Mjini kupitia chama cha CCM Khamis Sued Kagasheki. Kitu
kilichopelekea kurudiwa kuhesabiwa kwa kura zote na kupata uhakika wa
kutosha.
Kura zilizokubalika ni 54,211 sawa na
asilimia 98.54, kura zilizoharibika ni 805 sawa asilimia 1.46, Matokeo
ni kama ifuatavyo TLP kura 81 sawa na asilimia 0.2, ACT kura 453, Khamis
Sued Kagasheki wa CCM amepata kura 25,565 sawa na asilimia 47.2,
Wilfred Muganyizi Lwakatare wa Chadema amepata kura 28,112 sawa na
asilimia 51.9
Wafuasi
wa Chadema walionekana wakiwa wamekusanyika katika Ofisi za Halmashauri
Bukoba wakidai kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi wa huo wa Wabunge.
Vingozi
wa Chama cha Chadema wakiteta jambo, kushoto) ni Bw. Chief Kalumuna
Mshindi wa Udiwani Kata ya Kahororo aliyeshinda kiti hicho katika
Uchaguzi huu wa 2015. (Kulia) ni Mwenyekiti wa chama cha demokrasia na
maendeleo Chadema wilaya ya Bukoba Victor Sherejei.
Bw.
Wilfred Lwakatare kupitia Chama cha CHADEMA akiteta jambo na Diwani wa
Kata ya Kahororo kupitia Chama cha Chadema katika Ofisi za Halmashauri
ya Bukoba mjini huku wakisubiri matokeo ya Ubunge Bukoba Mjini.
Bw. Wilfred Lwakatare kupitia Chama cha CHADEMA
Mwenyekiti
wa chama cha demokrasia na maendeleo Chadema wilaya ya Bukoba Victor
Sherejei (kulia) mbele akiteta na Chief Kalumuna Diwani wa kata kahororo
wakibadilisha mawazo wakati wakisubiri matokeo usiku huu.
Waandishi wa habari na Makada wa Chama cha Chadema wakiwa katika Ofisi za Halmashauri ya Bukoba
Kidedea...Chif Kalumuna(kulia) wa Kata ya Kahororo akiwa amembeba mshindi bw. Wilfred Lwakatare
Wafuasi
wa Chadema walionekana wakiwa wamekusanyika kutaka kuvamia Ofisi za
Halmashauri ya Bukoba kudai kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi wa
wabunge na Polisi walikuwa tayari kuwakabili vilivyo na kuzuia umati huo
mkubwa.
Wafuasi wa Chadema wakitaka Matokeo yatolewa baada ya kuchukuwa muda tangu asubuhi mpaka jioni hii.
Taswira jioni hii maeneo ya karibu na Ofisi za Halmashauri.
Hapa
ikabidi kiongozi wa Chadema aliyeshinda katika Kata ya Kashai kupitia
chama hicho awatulize kwamba matokeo yanaenda kutolewa jioni hii.
Wafuasi wa Chadema wakitaka Matokeo
Wafuasi wa Chadema wakitaka Matokeo ya Kiongozi wao.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni