MEMPHIS DEPAY NA ROBIN VAN PERSIE WATOFAUTIANA LEOMAZOEZINI!
Mchezaji
wa Manchester United Memphis Depay amekwaruzana na Mchezaji wa zamani
wa Klabu hiyo Robin van Persie wakati wa mazoezi wa Timu ya Taifa ya
Netherlands. Tukio hilo limethibitishwa na Kocha wa Netherlands Danny
Blind lakini amepuuza umuhimu wake na imefahamika kuwa lilitokea kabla
ya Mechi ya Jumamosi ya EURO 2016 ambayo Netherlands iliifunga
Kazakhstan 2-1.
Kocha
Blind, ambae mwanawe, Daley, ni Mchezaji mwenzake Depay huko Man United
ambae pia yumo Timu ya Taifa ya Netherlands, alieleza: “Yapo matukio
mazoezini ambapo Wachezaji hutofautiana. Mnayazungumza. Na hivyo ndivyo
ilivyokuwa na yamekwisha.” Blind pia alisisitiza kuwa tukio hilo
halikumfanya ampige Benchi Van Persie kwenye Mechi na Kazakhstan ambayo
aliingizwa Kipindi cha Pili na kufikisha Mechi 100 kwa Nchi yake. Pia
Van Persie, ambae aliihama Man United Mwezi Julai kwenda Fenerbahce ya
Uturuki ukiwa ni Mwezi mmoja tu baada ya Depay kuhamia Man United, ndie
Mfungaji Bora wa Holland katika Historia ya Nchi hiyo akiwa na Bao 49.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni