Tagged Under:
JAKAYA MRISHO KIKWETE YOUTH PARK YAKARIBISHA VIJANA KUPIGA MECHI, MAZOEZI!
By:
Unknown
On: Jumanne, Oktoba 13, 2015
UONGOZI
wa Jakaya Mrisho Kikwete Youth Park umetoa mwaliko kwa Vijana wote na
Watanzania kwa ujumla kwenda kutumia Eneo hilo jipya na la kisasa
kabisa.
Uwanja huo upo Kidongo Chekundu katikati
ya Jiji la Dar es Salaam na umejengwa kutokana na kuhudi kubwa za Rais
wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, na kwa ushirikiano wa
Klabu ya Ligi Kuu England, Sunderland, na Kampuni ya Marekani ya
Nishati, Symbion.
Ndani
ya Eneo hilo upo Uwanja mkubwa wa kisasa wenye Kapeti la 3G pamoja na
Kiwanja cha kucheza Mechi za Timu za Wachezaji Watano dhidi ya Watano,
upo Uwanja wa Mpira wa Vikapu, Mpira wa Mikono na wa Magongo.
Viwanja vyote vina Taa za kutumika Usiku na yapo ya Majengo ya Menejimenti pamoja na Vyumba vya Kubadilishia Jezi.
Akitangaza
mwaliko huu kwa Vijana, Afisa Mwandamizi wa Utawala, Ismail A. Shah,
amesema Timu ambazo zitahitaji kufanya mazoezi au kucheza Mechi kwa
Kipindi cha kuanzia Saa 1 Usiku hadi Saa 4 Usiku, zipeleke maombi na
majina kamili ya Wachezaji/Washiriki.
Kwa maelezo zaidi Waombaji wametakiwa kuwasiliana na Namba ya Simu 0714436347.
0 maoni:
Chapisha Maoni