.

.

.

.

.

.

.

,

,

.

.

Jumapili, 11 Oktoba 2015

Tagged Under:

EURO 2016: ITALY, WALES, BELGIUM, ZAFANYA KWELI ZIPO FAINALI, UHOLANZI YANGOJEA MIUJIZA!

By: Unknown On: Jumapili, Oktoba 11, 2015
  • Share The Gag


  • Wales wamefanikiwa kutinga Fainali yao ya kwanza ya Mashindano makubwa tangu Mwaka 1958 baada ya Jana kufuzu kuingia Fainali za Kombe la Mataifa ya Ulaya, EURO 2016, licha ya kuchapwa 2-0 Ugenini na Bosnia.
    Wales wamefuzu kutoka Kundi B la EURO 2016 pamoja na Belgium ambao Jana waliinyuka Andorra 4-1 kutokana na Cyprus kuichapa Israel 2-1 katika Mechi nyingine ya Kundi hilo.
    Italy nao wamefuzu kutoka Kundi H baada ya kushinda Ugenini walipoichapa Ugenini Azbeijan Bao 3-1.
    Hadi sasa Timu 12, pamoja na Wenyeji France, zimeshatinga Fainali za EURO zikibakisha Nafasi 12 ambazo 8 zitajazwa kwa Mechi kati ya Leo na Jumanne na 4 zitatokana na Mechi 4 za Mchujo zikishirikisha Washindi wa 3 Bora wa Makundi ambazo zitachezwa Mwezi Novemba.
    Kutoka Kundi A, hali ni tete kwa Netherlands ambao Jana waliifunga Ugenini Kazakhstan 2-1 lakini wapo hatarini kuikosa Nafasi ya 3 kwa vile Turkey nao walishinda Ugenini kwa kuichapa Czech Republic 2-0.

    Toka Kundi A, Iceland na Czech Republic tayari zimefuzu na nafasi inayogombewa ya kwenda Fainali ni kupitia Tiketi ya Mshindi wa 3 ambayo Turkey watainasa wakitoka Sare na Iceland huko Uturuki Jumanne.
    Bao za Holland hapo Jana zilifungwa na Georginio Wijnaldum na Wesley Sneijder huku Straika wa zamani wa Manchester United akiingizwa Kipindi cha Pili kuichezea Holland Mechi yake ya 100.


    Katika Mechi ya mwisho hapo Jumanne, Holland watakuwa Wenyeji wa Czech Republic.

     
    TIMU ZILIZOFUZU HADI SASA [9 bado 15]:
    -France [Wenyeji]
    -KUNDI A: Iceland, Czech Republic
    -KUNDI B: Belgium, Wales
    -KUNDI C: Spain
    -KUNDI D:
    -KUNDI E: England, Switzerland
    -KUNDI F: Northern Ireland
    -KUNDI G: Austria
    -KUNDI H: Italy
    -KUNDI I: Portugal
    EURO 2016
    RATIBA
    Saa za Bongo
    Jumapili Oktoba 11
    1900 Armenia vs Albania
    1900 Faroe Islands vs Romania
    1900 Finland vs Northern Ireland
    1900 Greece vs Hungary
    1900 Serbia vs Portugal
    2145 Germany vs Georgia
    2145 Gibraltar vs Scotland
    2145 Poland vs Republic of Ireland
    Jumatatu Oktoba 12
    1900 Austria vs Liechtenstein
    1900 Russia vs Montenegro
    1900 Sweden vs Moldova
    2145 Belarus vs Macedonia
    2145 Estonia vs Switzerland
    2145 Lithuania vs England
    2145 Luxembourg vs Slovakia
    2145 San Marino vs Slovenia
    2145 Ukraine vs Spain
    Jumanne Oktoba 13
    2145 Belgium vs Israel
    2145 Bulgaria vs Azerbaijan
    2145 Cyprus vs Bosnia and Herzegovina
    2145 Italy vs Norway
    2145 Latvia vs Kazakhstan
    2145 Malta vs Croatia
    2145 Netherlands vs Czech Republic
    2145 Turkey vs Iceland
    2145 Wales vs Andorra

    0 maoni:

    Chapisha Maoni