
Martial akishangilia moja ya bao lake leo hii kwenye uwanja wa Southampton
Anthony Martial aliisawazishia bao Man United katika dakika ya 34 kipindi cha kwanza na kufanya 1-1. 
Mata akipongezwa baada ya kuipata bao la tatu Man United

Wakicheza
Ugenini huko Saint Mary, Manchester United Leo wameifunga Southampton
Bao 3-2 na kuchupa hadi Nafasi ya Pili kwenye Msimamo wa Ligi Kuu
England wakiwa Pointi 2 tu nyuma ya Vinara Man City.

Shujaa wa Mechi hii ni Chipukizi mpya Anthony Martial aliefunga Bao 2 na
la 3 kufungwa na Juan Mata huku Graziano Pelle akifunga Bao zote 2 za
Southampton.
Pelle alitangulia kuipa Southampton Bao katika Dakika ya 13 na Martial
kusawazisha Dakika ya 34 na kupiga Bao la Pili Dakika ya 50 na kufuatiwa
na Bao la Mata katika Dakika ya 68 huku Southampton wakifunga Bao lao
Pili kwenye Dakika ya 86.

Martial akishangilia bao lake la pili

Depay na martial wakipongezana
Anthony Martial dakika ya 50 aliiomgezea bao la pili Man United na kufanya matokeo kuwa 2-1.
3-1

Raha ya ushindi

Balaa!

Mata akitawanya mashabiki
Juan Mata alifanya 3-1 dhidi ya
Southampton dakika ya 68, Dakika ya 86 Graziano Pellé aliifungia tena
bao Southamton na kufanya 3-2 kwa bao la kichwa.
Sadio Mane akiendesha mbele ya Blind

Martial na Rooney wakijiuliza

Chalii!!

1-0
Graziano Pellé aanza kuipa bao Southampton mapema dakika ya 13 na kufanya 1-0.

Wamekutana Mameneja! Koeman na Van Gaal
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni