Nimepita kwenye page ya Facebook ya BBC Swahili nikakutana na hii stori ambayo nimeguswa kuishare hata hapa millardayo.com kuhusu nchi ya Ethiopia kuzindua Treni za umeme.

Ripoti inasema Treni hizi ambazo zimezinduliwa September 20 2015 zinaanza kubeba abiria na zinatarajiwa kurahisisha usafirishaji wa watu kwenye mji mkuu wa Addis Ababa, Ethiopia nchi ambayo mpaka mwaka huu wanasema idadi ya watu wake ni zaidi ya MILIONI 90.
BBC
wanasema hizi Treni zimetajwa kuwa mfano na za kwanza kusini mwa jangwa
la sahara ambapo ujenzi na uendeshaji wa huduma hii ya reli
unatekelezwa kwa ushirikiano na serikali ya China.
Picha zote ni kutoka BBC.
Treni
hizi za umeme zitakua na uwezo wa kuhudumia Abiria elfu kumi na tano
ndani ya dakika 60 ambapo Treni moja inaweza kubeba abiria 286 kwa
wakati mmoja.

Ripoti inasema Treni hizi ambazo zimezinduliwa September 20 2015 zinaanza kubeba abiria na zinatarajiwa kurahisisha usafirishaji wa watu kwenye mji mkuu wa Addis Ababa, Ethiopia nchi ambayo mpaka mwaka huu wanasema idadi ya watu wake ni zaidi ya MILIONI 90.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni