
Mechi yake ya kwanza kabisa ya Ligi kwa Martial, Kijana wa Kifaransa wa Miaka 19 tu, ilikuwa huko Old Trafford hapo Septemba 12 ambapo aliingizwa toka Benchi na kupachika Bao murua wakati Man United inaitandika Liverpool 3-1.
Hapo Jana, huku Man United wakiwa Bao 1-0 nyuma walipocheza na Southampton, Martial, akicheza Sentafowadi, huku Kepteni Wayne Rooney akiwa nyuma yake, ndie aliesawazisha Bao na kisha kupiga Bao la pili na Man United kwenda Bao 2-1 mbele.

Akimwongelea Martial, Mchezaji wa zamani wa Southampton, Morgan Schneiderlin, ambae Jana alirejea Saint Mary kuikabili Timu yake ya zamani kwa mara ya kwanza, alisema: “Kama mlivyomwona, ni mtulivu, hana mchecheto. Ana kipaji kikubwa. Amekuja Ligi Kuu England na anafunga. Ni Mchezaji mwenye akili mno, alietulia. Atakuwa Mchezaji Bora mno kwa Man United!”

Jumatano Man United ipo Old Trafford kucheza Mechi ya Raundi ya 3 ya Capital One Cup dhidi ya Ipswich Town na Jumamosi ijayo wapo tena Old Trafford kuivaa Sunderland kwenye Mechi ya Ligi Kuu England.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni