LIONEL MESSI ATWAA TUZO YA UEFA, NDIE BORA ULAYA MSIMU 2014/2015
Lionel
Messi ametwaa Tuzo ya UEFA ya Mchezaji Bora wa Ulaya kwa Msimu wa
2014/15 baada ya kushinda Kura zilizopigwa na Wanahabari toka Nchi 54
Wanachama wa UEFA. Messi, mwenye Miaka 28, ametwaa Tuzo hii kwa
kuwabwaga mwenzake wa Barcelona Luis Suarez na Mchezaji wa Real Madrid
Cristiano Ronaldo ambae ndie Mchezaji Bora Duniani.Hii
ni mara ya pili kwa Messi kutwaa Tuzo hii na mara ya kwanza ni Mwaka
2011 na safari hii ameibeba baada ya kuisaidia Klabu yake Barca kutwaa
Trebo yaani Ubingwa wa La Liga, Copa del Rey na UEFA CHAMPIONS LIGI. Washindi waliopita wa Tuzo hii ni Lionel Messi (2011), Andrés Iniesta (2012), Franck Ribéry (2013) na Ronaldo (2014).Taswira leo hii huko MonacoSuarez
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni