
Man United walikuwa tayari wameshakubaliana na Barcelona kuhusu Uhamisho wa Pedro ambae nae alishaafika maslahi binafsi na Man United lakini Dakika za mwisho Chelsea ikaingia na kumsaini.
Habari toka Old Trafford zilitoboa kuwa Meneja Louis van Gaal ndie alieamua kutomsaini Pedro baada kubainika uhusiano wake wa karibu na Mchezaji mwingine wa zamani wa Barcelona, Kipa Victor Valdes, ambae yuko Man United lakini sasa ana bifu kubwa na Van Gaal kiasi cha kutimuliwa toka Timu ya Kwanza na sasa kuwekwa kwenye Listi ya Wachezaji wanaouzwa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni