ARSENE WENGE AMLIA KIMYA KIPA WAKE PETR CECH, KIPIGO KUTOKA KWA HAMMERS CHALETA FIKRA NA PICHA TOFAUTI KWA WALIO WENGI!
.Huku
Wachambuzi wakimnyooshea kidole Kipa mpya wa Arsenal Petr Cech kwa
kufanya makossa yaliyoruhusa Bao zote walipopigwa 2-0 Leo kwao Emirates
na West Ham katika Mechi yao ya kwanza ya Ligi Kuu England kwa Msimu
mpya, Meneja Arsene Wenger amekataa kumshushia lawama Kipa huyo. Cech, alienunuliwa kutoka Chelsea, aliutokea Mpira wa Frikiki ili aupanchi lakini akaukosa na kutoa mwanya kwa Cheikhou Kouyate kufunga kilaini kwa Kichwa Bao la kwanza na kisha shuti la mbali la Mauro Zarate kumhadaa Cech kwenye Posti yake ya karibu na kutinga.
Lakini
Wenger, akiongea mara baada ya kipigo hicho, ameeleza: “Ni kutokuwa
makini kwa pamoja. Kuna vitu vingi hapo. Nilijua kama ile frikiki
itapigwa vizuri basi tutakuwa mashakani kutokana na tulivyojipanga,
tulijiua wenyewe. Sijaongea na Cech lakini sikuona Mchezaji mwingine
yeyote akicheza kwa kufurahisha hii Leo hivyo ni ngumu kumlaumu mmoja.”
Aliongeza: “Pasi zetu hazikuwa nzuri. Leo lazima tujitazame wenyewe. Hatukuwa wazuri.” Mara baada ya Wikiendi iliyopita kuwafunga Mabingwa Chelsea Bao 1-0 huko Wembley na kutwaa Ngao ya Jamii, Wachambuzi wengi huko England waliipa nafasi kubwa Arsenal kuwemo rasmi kwenye kinyang’anyiro cha Ubingwa Msimu huu lakini kichapo hiki cha Leo kimeleta fikra nyingine.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni