.

.

.

.

.

.

.

,

,

.

.

Jumatatu, 6 Julai 2015

Tagged Under:

OKWI ATIMKIA DENMARK KWA MAJARIBIO, SIMBA YATOA BARAKA ZOTE

By: Unknown On: Jumatatu, Julai 06, 2015
  • Share The Gag

  • MSHAMBULIAJI wa Simba Emmanuel Okwi anatarajiwa kuondoka kwenda nchini Denmark katika klabu ya Sonderjyske iliyopo kwenye Danish Superliga. Majaribio hayo yatakuwa ya siku 14 kuanzia tarehe 08/07/2015 na baada ya hapo klabu hiyo ya Sonderjyske itatuma ripoti kamili ya majaribio yake.
    Tovuti ya Simba imemnukuu Rais wa klabu, Evans Aveva akisema; “Simba inafurahi sana kuona wachezaji wake wanapata nafasi hizi za kuonesha vipaji vyao tena kwenye viwango vya kimataifa zaidi, hivyo Simba inamtakia kila la kheri Okwi kwenye majaribio yake ya siku 14 kwnye klabu ya Sonderjyske iliyopo kwenye Danish Superliga”.
    Okwi alizaliwa Desemba 25, 1992 Kampala Uganda anachezea timu ya Taifa ya Uganda kama mshambuliaji wenye jezi namba 10.

    0 maoni:

    Chapisha Maoni