KOCHA MKUU BONIFACE MKWASA AWASHUKURU WATANZANIA, ATAKA APEWE MUDA ZAIDI KUITENGENEZA TIMU YA TAIFA!
Kocha
Mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) inayodhaminiwa na bia
ya Kilimanjaro Premium Lager, Charles Boniface Mkwasa amewashukuru
watanzania wote waliowapa sapoti katika mchezo wa marudiano dhidi ya
Uganda uliochezwa mwishoni mwa wiki jijini Kampala. Mkwasa amesema
kujitolea kwa wachezaji wa Taifa Stars (uzalendo) katika mchezo huo
kulipelekea kuwapa wakati mgumu wenyeji, huku watanzania waliojitokeza
kuja kushuhudia mchezo huo wakiwashangilia muda wote wa mchezo. “Kiukweli
japo timu haikuweza kupata matokezo mazuri sana, lakini tunamshukuru
mungu ndani ya wiki moja ya maandalizi, tumeweza kuwapa maelekezo vijana
na kuyafanyia kazi, japo wengine walikua wakicheza kwa mara ya kwanza
timu ya Taifa walicheza vizuri, kijumla wote kwa pamoja walifanya vizuri
sana katika mchezo dhidi ya Uganda” alisema Mkwasa. Aidha
Mkwasa amesema kwa sasa wataomba kupata nafasi ya japo siku 10 kufanya
mazoezi kwa pamoja kujiandaa na mchezo wa kuwania kufuzu kwa Fainali za
Mataifa Afrika (AFCON) dhidi ya Nigeria Septemba 5 mwaka huu, na
kuwaomba watanzania wote kuwaunga mkono katika maandilizi hayo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni