
Mkurugenzi
wa Mawasiliano na Masoko wa Kampuni ya Mawasiliano na
Masoko,Consitantine Magavila akizungumza na waandishi wa habari leo
katika ukumbi wa Idara ya habari MAELEZO jijini Dar es Salaam.kutoka
kushoto ni msanii wa Bongo Fleva George Mdemu (Gnako),Afisa mipango wa
kampuni ya Open Society Intiative for Eastern Africa(OSIEA),Adam
Antony,Afisa Elimu NEC,Rose Malo pamoja na Snura Mushi(Snura).

Afisa
Elimu wa NEC,Rose Malo akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na
vijana walioona umhimu wa kupiga kura na kuhamasisha vijana wengine kwa
njia ya nyimbo,kutokana na mwaka huu kuwa ni mwaka wa Uchaguzi mkuu hapa
nchini akizungumza katika ukumbi wa Idara ya habari maelezo jijini Dar
es Salaam leo. kulia ni Mkurugenzi wa Mawasiliano na Masoko wa Kampuni
ya Mawasiliano na Masoko,Consitantine Magavila na Afisa mipango wa
kampuni ya Open Society Intiative for Eastern Africa(OSIEA),Adam Antony.
kutoka kushoto ni msanii wa Bongo Fleva George Mdemu (Gnako), Snura
Mushi (Snura),Kala Masanja (Kala Jeremiah) pamoja na Boniventure
Kabogo(Stamina) wakiimba kipande cha wimbo ambao utakuwa ukielimisha
jamii kuhusiana na umhimu wa upigaji kura katika uchaguzi mkuu
utakaofanyika Oktoba mwaka huu.
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
VIJANA wamekuwa na changamoto ya
kutoshiriki katika zoezi la kujiandikisha katika daftari la kudumu la
mpiga kura na kushindwa kupata haki yake msingi ya kupiga kura katika
chaguzi mbalimbali zinazofanyika nchini.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni