PHIL JONES ASAINI MKATABA MPYA MANCHESTER UNITED.
Phil
Jones, mwenye Miaka 23, amesaini Mkataba mpya na Man United ambao
utambakiza Klabuni hapo hadi Juni 2019 pamoja na nyongeza ya Mwaka mmoja
juu yake.
Jones alianza kuichezea Man United Mwaka 2011 na
ameshacheza Mechi 128 na kutwaa Ubingwa wa Ligi Kuu England mara moja
Mwaka 2013.
Akiongea
baada ya kusainiwa Mkataba huo mpya, Meneja Louis van Gaal alisema:
"Tumefurahi Phil amesaini Mkataba mpya. Yeye ni Mchezaji mwenye kipaji
anaeweza kucheza nafasi nyingi. Bado ni Kijana anae endelea wakati
wote."
Nae Phil Jones ameeleza: "Nimefurahishwa kusaini dili mpya. Hii ni Klabu kubwa kushiriki nayo na naungoja kwa hamu Msimu mpya."
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni