Norwich
City Leo hii wamefanikiwa kurudi tena Ligi Kuu England baada ya
kuporomoka Msimu mmoja uliopita baada ya kuichapa 2-0 Middlesbrough
kwenye Fainali ya Mchujo wa Timu 4 za Daraja la Championship iliyochezwa Uwanjani Wembley Jijini London.
Mbele
ya Watazamaji 85,656, Norwich City walipiga Bao zao 2 ndani ya Robo Saa
ya Kwanza kwa Bao za Cameron Jerome alietumia vyema makosa ya Daniel
Ayala na kufunga na kisha katika Dakika ya 15 Nathan Redmond alipiga Bao
la Pili.
Norwich
City, ambao walimaliza Ligi ya Championship Nafasi ya 3 na hivyo kukosa
nafasi ya kupanda Ligi Kuu England moja kwa moja, kwenye Nusu Fainali
ya Mechi hizi za Mchujo waliibwaga Ipswich Town Jumla ya Mabao 4-2
katika Mechi mbili.
Boro walitinga Fainali hii kwa kuichapa Brentford Jumla ya Mabao 5-1 katika Mechi mbili.
Norwich
City sasa wameungana na Bournemouth na Watford, ambazo zilimaliza
Nafasi mbili za juu za Ligi ya Championship na kupanda Daraja moja kwa
moja, kucheza Ligi Kuu England Msimu ujao kuzibadili Hull City, QPR na
Burnley zilizoporomoka Daraja.
Mashabiki wa Boro

Timu zikiingia Uwanjani Wembley

Kikosi cha Norwich

Kipute kimeanza ...mchezaji wa Boro chini

Jerome ndie aliyeanza kufunga bao la kwanza

Jerome akishangilia bao lake la kwanza

Meneja wa Noewich Alex Nail akishangilia nae

Nathan Redmond alipachika bao la pili

Wafungaji wakakutana live Nathan na Jerome

Wachezaji wa Boro hoi!!

Mashabiki nao wakazimika!!

Taswira Meneja wakiwajibika Uwanjani!

Jerome alipumzishwa!

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni