DANIEL STURRIDGE AFANYIWA UPASUAJI NCHINI MAREKANI..SASA KURUDI UWANJANI MSIMU UJAO!
Mshambuliaji
wa klabu ya Liverpool, Daniel Sturridge amefanyiwa upasuaji, akiwa
Nchini Marekani kwa lengo la kumaliza tatizo la majeraha ya paja ambayo
yamemsababishia kuwa nje ya uwanja katika kipindi hiki cha kuelekea
mwishoni mwa msimu wa 2014-15.
Sturridge yupo nchini Marekani tangu
Ijumaa lililopita na amewathibitishia hilo mashabiki kwa kuweka picha
kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram.
Inaaminika kwamba hatua ya kufanywa kwa
upasuaji huo, itamuwezesha Sturridge kuwa katika hali nzuri ya kucheza
kwa kujiamini kuanzia mwanzoni mwa msimu huu, baada ya kupata wakati
mgumu katika kipindi cha msimu huu.
Meneja
wa klabu ya Liverpool, Brendan Rodgers, anatarajia kuwa sanjari na
mshambuliaji huyo wakati wa maandazlii ya msimu wa 2015-16, ambapo The
Reds watafanya ziara nchini Australia pamoja na Malaysia.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni