Kikundi mahiri cha KAPOTIVE Star Singers kutoka Mjini Bukoba leo kimefanya Tamasha kubwa la Pasaka kwenye Mji wa Geita katika Ukumbi wa GEDECO na kushuhudiwa na Umati wa Watu wengi zikiwemo Kwaya mbalimbali za hapa Geita na Waumini mbalimbali na kuifurahia Pasaka hiyo ambayo ni Alama ya Ukombozi wa Mwanadamu dhidi ya Dhambi kupitia kifo na Ufufuko wa Yesu Kristo. Wana'KAPOTIVE walisindikizwa na kwaya ya Mt. Thomas wa Aquino na Aaron Entertainment wa hapo Geita. Watu walivutiwa sana na kiwango cha juu ya kikundi cha KAPOTIVE mpaka wengine wakadiriki kusema sio kutoka Bukoba.



Hakuna maoni:
Chapisha Maoni