LIGI KUU VODACOM KUENDELEA JUMAMOSI, KAGERA SUGAR v SIMBA, NDANDA FC v MBEYA CITY
Ligi
Kuu ya Vodacom inatarajiwa kendelea kutimua vumbi mwishoni mwa wiki
katika sita nchini, kwa michezo minne kucheza siku ya jumamosi na
michezo mwiwili kuchezwa siku ya jumapili.
Jumamosi uwanja wa
Kambarage mjini Shinyanga, Kagera Sugar watakuwa wenyeji wa Simba SC
kutoka jijini Dar es salaam, huku jijini Tanga Coastal Union
wakiwakaribisha maafande wa jeshi la Magereza nchini Tanzania Prisons
kwenye Uwanja wa Mkwakwani.
Ndanda
FC ya Mtwara watakuwa wenyeji wa wagonga nyundo timu ya Mbeya City
katika uwanja wa Nagwanda Sijaona, wakati maafande wa Jeshi la Kujenga
Taifa Ruvu Shooting wakicheza na ndugu zao JKT Ruvu katika uwanja wa
Mabatin uliopo Mlandizi.
Siku ya jumapili Stand United
watawakaribisha wakata miwa kutoka Morogoro Mtibwa Sugar kwenye uwanja
wa Kambarage, huku Mgambo Shooting wakiwa wenyeji wa timu ya Polisi
Morogoro kwenye uwanja wa Mkwakani jijini Tanga.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni