VODACOM PREMIER LEAGUE KUENDELEA WIKIENDI HII, COASTAL UNION vs KAGERA SUGAR, SIMBA SC vs YANGA
Ligi
Kuu ya Vodacom inatarajiwa kuendelea mwishoni mwa wiki kwa viwanja sita
kutimua vumbi, michezo mitatu ikifanyika siku ya jumamosi na michezo
mingine mitatu kufanyika siku ya jumapili.
Katika Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro, wenyeji timu ya Polisi
Morogoro watawakaribisha maafande wa Ruvu Shooting kutoka Mlandizi,
Coastal Union watakua wenyeji wa Kagera Sugar kwenye dimba la Mkwakwani,
huku JKT Ruvu wakiwakaribisha Azam FC katika uwanja wa Azam Complex
Chamazi. Jumapili Mgambo JKT watakua wenyeji wa timu ya Ndanda FC
kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga, huku Mtibwa Sugar wakiwa
wenyeji wa wagonga nyundo timu ya Mbeya City katika Uwanja wa Manungu
Turiani. Katika
Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam watani wa jadi Simba SC watakuwa
wenyeji wa Young Africans, mchezo unaotarajiwa kuanza kutimua vumbi
majira ya saa 10 kamili jioni kwa saa za Afrika Mashariki.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni