CHELSEA BAADA YA KUTUPWA NJE UEFA CHAMPIONS LEAGUE, KOCHA JOSE MOURINHO ATAMBA KUIBUKA NA UBINGWA WA LIGI KUU ENGLAND MSIMU HUU.
Chelsea itatwaa Ubingwa wa Ligi Kuu England Msimu huu kwa mujibu wa Meneja wao makeke Jose Mourinho. Juzi Jumatano Chelsea ilitupwa nje ya
UEFA CHAMPIONS LIGI na Paris St-Germain lakini kwenye Ligi Kuu England
wao ni Vinara wa Ligi wakiwa Pointi 5 mbele ya Timu ya Pili Manchester
City ambao ni Mabinngwa Watetezi waliocheza Mechi 1 zaidi. Leo,
akiongea na Wanahabari kwa ajili ya Mechi yao ya Ligi yaJumapili dhidi
ya Southampton itakayochezwa Uwanjani Stamford Bridge, Jose Mourinho
amesema: "Watu waliotolewa Jumatano ndio hao hao ambao wako juu kwenye
Ligi tangu ya Siku ya kwanza. Ndio hao hao waliotwaa Capital One Cup na
ndio hao hao watatwaa Ligi Kuu!"Diego akiwa chini ya ulinzi mkali wa beki David Luiz.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni