WAYNE ROONEY ALILIA USHINDI DHIDI YA SUNDERLAND JUMAMOSI! ASEMA NI MUHIMU KUIFUNGA ILI WACHEZE KLABU BINGWA ULAYA
NAHODHA
wa Manchester United ametamka kuwa baada ya kufungwa na Swansea City
basi hawana budi kuifunga Sunderland Jumamosi la sivyo wataikosa UEFA
CHAMPIONS LIGI. Jumamosi, wakicheza huko Liberty Stadium, Man United
waliongoza Bao 1-0 lakini wakairuhusu Swansea kuwachapa Bao 2-1 kikiwa
ni kipigo chao cha pili katika Mechi 20 zilizopita chini ya Meneja Louis
van Gaal. Ingawa
bado zipo Mechi 12 hadi Msimu wa Ligi Kuu England kunamalizika, lakini
Mechi zao 7 baada ya Sunderland Jumamosi hii ni dhidi ya Tottenham na
Liverpool, zinazowania 4 Bora kama wao, pia dhidi ya Manchester City na
Chelsea ambazo ndizo ziko kwenye mbio za Ubingwa Msimu huu na pia dhidi
ya Everton inayozidi kuimarika baada ya kuyumba. Hali
hiyo imemfanya Kepteni Wayne Rooney kupiga Mbiu ya Mgambo kwamba
ushindi Jumamosi hii inayokuja dhidi ya Sunderland Uwanjani Old Trafford
ni kitu cha lazima. Kepteni
Rooney ametamka: “Tunahitaji kulipa Mechi ijayo. Ni Gemu ambayo ushindi
ni lazima. Tunatakiwa kushinda ili turudi kwenye reli na kuanza mbio
nyingine za ushindi tumalize 4 Bora!”Luis Van Gaal akitoka Uwanjani baada ya kubamizwa bao 2-1 na Swansea City Wachezaji wa Swansea City wakishangilia baada ya kuibamiza United hivi karibuni.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni