Habari hizi zimetobolewa na Wakala wa Kipa huyo kutoka Spain, Jorge Mendes, ambae ametupilia mbali dhana kuwa amekubaliana na Real Madrid kujiunga nao.
Hivi sasa De Gea, mwenye Miaka 24 na ambae pia ni Kipa wa Timu ya Taifa ya Spain, amebakiza kama Miezi 18 kwenye Mkataba wake na Man United na hilo lilianzisha uvumi mkubwa kuwa ataenda Real Madrid.

De Gea ni Mzaliwa wa Jiji la Madrid na alianza kuichezea Atlético Madrid tangu akiwa na Miaka 13 kisha kuichezea Timu ya Kwanza kwa mara ya kwanza Mwaka 2009 na Mwaka uliofuatia alikuwa langoni wakati Atletico inatwaa UEFA EUROPA LIGI na UEFA SUPER CUP.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni