

Hata hivyo, chimbuko la habari hizi zimedai ili kumpata Hummels itabidi Man United walipe zaidi ya Pauni Milioni 32 Dau ambalo litazidi lile la Man City walipolipa kiasi hicho kumnunua Eliaquim Mangala kutoka FC Porto mwanzoni mwa Msimu na kuweka Rekodi ya kuwa Beki ghali huko Uingereza.

Klabu ya Hummels, Dortmund, hivi sasa inasuasua kwenye Bundesliga ikiwa nafasi ya 4 toka mkiani ikiwa na Pointi 10 tu baada ya Mechi 11 za Ligi.
Akiongea na Wawekezaji Jumanne iliyopita, Ed Woodward alitamka: “Hatuingii Sokoni kusaka viraka vya muda mfupi. Lakini tunao walengwa tunaowataka mwishoni mwa Msimu. Ikitokea yeyote kati yao atapatikana Januari, kitu ambacho adimu, sisi tutamchukua!”
Ikiwa Hummels atapatikana, hilo litawasaidia sana Man United wenye Difensi dhaifu na Wachezaji wanaokumbwa na majeruhi ya mara kwa mara kina Chris Smalling, Phil Jones na Jonny Evans.
Mbali ya Hummels, pia zipo taarifa kuwa Van Gaal anamnyemelea Kiungo wa Holland anaechezea AS Roma, Kevin Strootman, ambae hivi karibuni alirejea Uwanjani na kuingizwa kutoka Benchi wakati AS Roma inaichapa Torino 3-0 baada ya kuwa nje kwa muda mrefu akijiuguza Goti lake
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni